Mpendwa katika Bwana, wiki ilyopita nilianza somo linalohusu kiongozi bora wa kiroho vile anavyopatikana. Na sasa tutaendelea na somo hili. Kabla hatujaendelea nikutakie kila la kheri kwa kuuanza mwaka mwingine wa 2018. Najua kuwa unamipango mizuri mno kwa mwaka huu Bwana Mungu akufanikishe na kukubariki.
Kalibu sasa tuendelee na makala yetu kuhusu kiongozi bora wa kiroho. Kiongozi bora wa kiroho ni yule anaejitoa kwa moyo wa upendo, kuwatumikia anao waongoza bila kulazimishwa. Uongozi wa kiroho siyo kutawala watu, na kuwaamlisha kutii matakwa yako binafsi. Bali uongozi wa kweli wa kiroho ni kuwaelekeza watu kwa moyo wa upendo, bila kuangalia hali zao kielimu na kiuchumi.Hata kama ungelikuwa na elimu ya juuu kiasi gani. Yesu kristo alikuwa na theolojia kubwa ya mbinguni lakini alihitaji kushilikiana na watu wasiokuwa na elimu kabisa akawaita wanafunzi lengo lake kuwaongoza kwa kuwaelekeza ili wamjue Mungu kupitia yeye. Na wao wawaongoze wengine kwa roho ya upendo ili wamjue Mungu wa upendo.
Kwa kifupi kiongozi ni mtumwa wa wale anaowaongoza Akawambia wafalme wa mataifa huwatawala, na wenye mamlaka juu yao huitwa wenye fadhili; lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye. Maana aliye mkubwa ni yupi? yeye aketiye chakulani au yule atumikaye? siye yule aketie chakulani?Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye. Luk 22:25,27). Maudhui ya misitari hii, inaonyesha wazi kabisa kwamba mafundisho ya Yesu, hayakuwa katika utawala wa kujionyesha na kutumia madaraka. Bali alimaanisha uongozi wa kiroho ni cheo cha chini mno kina chofananishwa na mtu mwenye kuchunga wanyama /kondoo. Katika desturi ya kiyahudi mchungaji, alionekana ni mtu wa kawaida tu katika jamii. Kiongozi wa kiroho husimama kama mchungaji anayechunga na kulinda kundi (kanisa) ambalo siyo lake ni la Bwana wake yeye ni mtumishi tu kristo ndiyo mwenye mali hii yeye ndiyo hukusanya na kumkabidhi mwangalizi ili awaangalie siyo kuwatawala na kuwaumiza. Mchungaji kamwe hawezi kusababisha wokovu kwa matendo yake na juhudi zake binafs kwa watu. Watu huokolewa na kristo na kufundishwa na Roho mtakatfu ili wamjue Mungu na kanuni ya Mungu ya kutunza wokovu. Mchungaji au kiongozi kazi yake ni kusimamia kanuni za Mungu chini ya muongozo wa Mungu ambao ni neno la Mungu (biblia) siyo maneno ya mchungaji/ kiongozi ama tabia ya mchungaji.
Shida kubwa leo katika kanisa la Mungu viongozi wengi wanaingia kuongoza wakiwa na hamu kubwa ya kujilimbikzia mali wala si kuongoza. makanisa mengi yamekuwa mitaji yao ya kuwaingizia vipato. Leo ni jambo la kawaida tu mchungaji na mchungaji kuhonga ili apate nafasi ya uongozi wa juu au kugombana kwa ajili ya muamini mmoja eti kahamia kanisa jingine kwa kuwa ana nafasi ya pesa. swala kugombania madaraka limekuwa ndiyo agenda. Jamani hakuna mchungaji au kiongozi aliyeumba mtu watu wote ni wa Mungu siyo watu wetu sisi ni wasimamizitu na mpango wa Mungu, kila mtu atasimama mbele ya kiti cha hukumu haijalishi ni mchungaji au mshilika wa kawaida. Leo hii mtu asipotoa sadaka ya kumlidhisha mchungaji,anaonekana hana lolote, hafai, amelaaniwa, hana faida nk hata kama angekuwa na huduma fulani anaaza kutafutiwa mbinu ya kushushwa kihuduma. Uongozi wa namna hii hautokani na Roho mtakatifu bali hutokana na tabia binafsi ya mtu na matakwa yake binafsi .
Sehemu inayofuata nitaongelea tabia ya kiongozi wa kinafsi na kiongozi wa kiroho asante.....
Monday, 1 January 2018
New
Kiongozi bora wa kiroho;
About mponeja bloger
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment