Kiongozi bora wa kiroho ni Yule anayejitoa
kwa moyo wa upendo kuwatumikia anaowaongoza bila kulazimishwa. Uongozi wa
kiroho siyo kutawala watu. Na kuwaamrisha watu kutii matakwa yako binafsi. Bali
uongozi wa kweli wa kiroho ni
kuwaelekeza watu kwa moyo wa upendo bila kuangalia hali zao na haliyako kwamba
unawazidi nini. Kwa kifupi kiongozi ni mtumwa wa wale anaowaongoza. Akawabia
wafalme wa mataifa huwatawala, na wenye mamlaka juu yao huitwa wenye fadhili;
lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na
mwenye kuongoza kama Yule atumikaye. Maana aliye mkubwa ni yupi? yeye
aketiye chakulani, au Yule atumikaye? Siye Yule aketie chakulani? Lakini mimi
kati yenu ni kama atumikaye. Luk 22:25,27]. Yesu alimaanisha kiongozi asiwe
mtu mwenye kujisikia kuwa yeye ni kiongozi bali alitaka kiongozi awe ni mtu
anayejiona kuwa ni mtumwa maana yake ni mtu aliyetumwa kwa watu wasio wake.
Tukijua hilo hatutajiinua na utumishi wetu utakuwa safi mbele za Bwana.
Ingawaje biblia inazungumza kuhusu
kuonya, kukemea, na kukalipia lakini si
katika ukatili wa kibinadamu wenye asili ya ubinafsi na kutosemehe uletao
uadui.
Maneno haya karipia, kemea, na onya katika biblia
hayamaanishi kufoka , kuwa na jaziba
Fulani, kuwa na hasira na mtu furani kwa sababu ya makosa aliyoyafanya nk. Bali
humaanisha kuelekeza kwa kina kupitia
neno la Mungu. Ukiangalia kwa kina Paulo, anavyotoa maelekezo kwa Timotheo,
madhui ya waraka huu huonyesha kabisa Paulo alitaka Timotheo ahubiri na kufundisha neno la kristo kwa uvumilivu wote. Lihubiri neno uwe tayari wakati
ukufaao na wakati usio kufaa karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na
mafundisho. 2)Tim 4:2,3}.Katika lugha ya asili |kiyunani| maneno haya
humaanisha kusihi, kushawishi mtu ahame toka kwenye tabia au mazingira
aliyoyazoea, kutoa tahadhari ya mambo yatakayompata mtu mwenye tabia ya asili
asipobadilika. Katika tafsiri ya kiyunani cha kisasa, misitari hii humaanisha
hivi,hubiri
huo ujumbe, sisitiza kutangaza iwe ni wakati wa kufaa au wakati usio faa
karipia, onya na himiza….. Kiongozi wa kweli hachaguliwi kwa muonekano
wan je tu kuwa anafaa au kwa elimu yake tu ya darasani.
Bali kiongozi wa kiroho huchaguliwa na
utatu mtakatifu wa Mungu.Ingawa Mungu anaweza kutumia watu kuchagua kiongozi,
lakini lazima Roho mtakatifu aliye kiongozi mkuu apewe nafasi ya kusema na watu
na kuwahakikishia kwamba mtu huyu anafaa kuwa kiongozi. Kiongozi wa kiroho
hawezi kupatikana paspo Roho mtakatifu. Tunapomluhusu Roho mtakatifu na kumpa
nafasi ndani ya roho zetu, yeye huingia na kufanya makao ndani mwetu. Kazi yake
kubwa ni kubadili utu wetu wa asili ya dhambi na kutuzaa upya kwa imani nafsi
zetu zilizokuwa zimehalibiwa na shetani zinahuishwa na kumtii kristo. Tabia
zetu na matendo yetu ya asili yanakufa[M1] [M2] [M3] yaani uchoyo, majivuno,kiburi chuki,
unafiki na kila aina ya ubaya yanaondoka kabisa.
Zaidi ya hayo utajipatia katika
watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye
kuchukia mapato ya udhalumu; ukawaweke juu yao, wawe wakuu…..kut 18:21,22]. Taz
mdo 6:3,6].
Neno hili
kiongozi kwa lugha ya asili yaani
kule biblia ilikoanzia /kiyunani humaanisha kiongozi ni mtu anayesahau au
kuacha mambo yake au kazi zake kwa ajili ya w engine hii huonyesha ni mtu asiye
angalia masirahi katika kazi yake. Tangu mwanzo neno kiongozi,
lilitafsiliwa kuwa ni Masihi.Lilitokana na lugha ya kiebrania
likimaanisha ‘’mpakwa mafuta’’ neno hili
lilitumika kwa wale tu waliokuwa wamechaguliwa na Mungu kwa ajili ya kuwaongoza
watu wa Mungu. Waisraeli wa agano la kale, walifanya sherehe ya kupaka mafuta
kwa wafalme, makuhani, na mara nyingine kwa manabii mafuta rasimi yalimiminwa kichwani pa mtu
ikiwa ishara ya kuwa tangu sasa amekuwa na haki ya kuwa kiongozi, ili
kutekeleza huduma iliyolingana na wito wake. Taz kut, 28:41]. 1]fal 1:39. Na
19:16].
Katika nchi za agano jipya
zilizokuwa na lugha ya kiyunani, neno la kiebrania ‘’masihi’’ lilitafsiriwa katika kiyunani likawa ‘’kristo” likimaanisha
mpakwa mafuta. Hii haimaanishi kwamba kiongozi achukue nafasi ya kristo na
kulitumia jina hili kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya kufanya lolote kwa wale
anaowaongoza la bali humaanisha kiongozi wa kiroho anatakiwa kuwa wakili bora
anayemuwakilisha kristo katika uogozi bora . Tabia na mwenendo wake uwe kama wa
kristo. Asitake madaraka kwa manufaa yake na familia yake.
Migogoro
mikubwa makanisani, siku hizi inaletwa na viongozi. Viongozi wanaojiita
maasikofu na wachungaji, asilimia kubwa ya watu hawa wamekuwa chachu ya
maendeleo ya kanisa wamechachua mpaka waumini
kwa kuwaingizia roho za uadui. Mchungaji na mchungaji hawapatani
wanawalazimisha na wanaowaongoza wawe na chuki
juu ya mchungaji Fulani wakitumia
sentesi dhaifu kabisa mimi naita sentesi mfu eti wanasema mimi ni baba yenu na
ninyi ni wanangu baba akisema lolote mtoto lazima utii na kukubali. Viogozi
hawa wanatia huruma kwani kanisa wanakolipeleka si huko kristo anakotaka. Badala
ya kutengeneza na kuzalisha viongoz I bora wa kesho wao wanatengeneza
nakuzalisha kesi nyingi sana mahakamni zisizokuwa na maana yoyote. Wana hujumu
mali za kanisa bila hata hofu ya Mungu wanataka wapewe heshima za kichungaji na za kiasikofu wanatanguliza
vyeo vyao mbele kuliko kumtanguliza kristo kwa nje ni watumishi wa Mungu lakini
ndani ni mafasayo wakubwa. Tena matendo yao yote huyatenda ili watazamwe na
watu. Ni watu wanaopenda kutumia vyeo vyao. Hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi
mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu Rabi…….Math
23:6,12). Ukiangalia sura nzima ya 23 katika mathayo, mwandishi
ananukuru kwa kina mafundisho ya Yesu yanayokemea tabia ya watu wanaotaka kutumia
madaraka ya uongozi kwa kuwafanya wengine kama mateka. Hawako tofauti na
wandishi na mafarisayo wanafiki Ole wenu wandishi na mafarisayo, wanafiki
kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni;[kwa kuwawekea masharti
magumu]..ninyi wenyewe hamuingii, wala wanaoingia [washrika waliodhamilia]..hamuwaachi
waingie. Utakuta mchungaji ameweka mashariti kibao kanisani kwake
utadhani anongoza familia yake washirika wanamhofu na kumtetemekea kuliko hata
Mungu wanaona ni afadhali kumkosea Mungu
kuliko mchungaji. Mchungaji mwema huwafanya watu kuwa rafiki ili wamueleze
matatizo na udhaifu wao unaowafanya kushindwa kuwa wakamilifu mbele za Bwana
ili auchukue mbele za Bwana kwa maombi siyo kufoka tu na kuwatishia laana.
Mchungaji mmoja alitumia dakika30 madhabahuni akimfokea mshirika mmoja alipitia
mlango wa pembeni anaotumia mchungaji kuingia kanisani baada ya ibaada mtu huyo
hakuludi tena kanisani na mchungaji hakuonekana wala kuumiza kichwa chake kwa
ajili ya mshirika huyo kilchofaata ni mchungaji huyo kusema huyo ni mpagani
kabisa. Ni vizuri kuwa na utaratibu, katika ibaada zetu lakini masherti
yasitufanye kuwakosesha wengine wasmwabudu Mungu kwa furaha na amani kwa kigezo
kuwa eti wewe ndiyo mchungaji eti hata
kama nibaki peke yangu kazi itaenda tu hapana. Tangu mwanzo Mungu wetu ni wa
watu wengi kwa nini asingekomea na Adamu peke yake aliyemuumba lakini akataka
kupitia Adamu watu wakaongezeke na kuijaza nchi.
Wala msiitwe viongozi; kiongozi wenu ni
mmoja naye ndiyo Kristo Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu,
23:10,12). Siyo kwamba atakuwa baba yenu kama watu walivyolibadilisha
neno hili na kujiita mababa wa kanisa. Makusudi ya sura hii nzima yanapatikana
kwenye mstari wa 12. Ingawa Yesu alisema maneno mengi kuwaonya viongozi
waliokuwa wakiwabebesha wengine mizigo mizito na wao hawawezi kuibeba,
wanajihesabia haki siku zote, msingi na kusudi kuu la mafundisho yake lilikuwa
ni hili hapa. Na yeyote atakayejikweza, atadhiliwa; na yeyote atakayejidhili,
atakwezwa 23:12).
Maneno haya yesu anazungumza juu ya
viongozi sio washirika. Ingawa alikuwa anazungumza na viongozi wa sheria,
asilimia kubwa ya wachungaji wa leo, ndiyo wanayafanya hayo wamekuwa
wakandamizaji wakubwa wa washrika na wachungaji wenye huduma ndogo bila hata
msaada wowote wakijisema wanasimamia maadili ya wokovu. Lakini bado wanatapeli
mali za washirika na kujitangaza wamebarikiwa na Mungu. Kama ni Mungu kwa nini
aswabariki na hao wanao leta sadaka?. Angalia kisa cha mchungaji mmoja wa
kanisa furani la kipentekoste
Alimuita mzee wa kanisa ofisini kwake
akitaka kumtuma dukani kwakuwa mchungaji huyu alitaka kitu hicho kiwahi, mzee
wa kanisa kwa kuwa alikuwa wa makamo, aliangalia kijana mwepesi ili akimbie
haraka na kuludi. Baada ya mda kidogo mchungaji alitoka nje akmuita na
kumuuliza Yule mzee na yeye mzee hakuwa na wasiwasi akajibu akajibu akasema
nimemwagiza kijana ili awahi. Mchungaji
alimnasa kofi la shavu kwakuwa mzee huyu hakuwa na maadalizi ya kichpo hicho
alishika shavu lake kwa maumivu makali mbele ya watu, akazunguka nyuma ya jengo la
kanisa. Hii yote ni kujiona kuwa mimi ni kiongozi. Sifa wanayotakiwa kuwa nayo
wafuasi wa kristo ni utumishi siyo kutumikiwa.
Kiongozi wa kanisa, mwenye kazi ya uchungaji, ambao ni tofauti na mashemasi huitwa mhudumu
pia. Naye
alitoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa
wainjilisiti; na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha [siyo kuwasambaza]..watakatifu,
hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa kristo ujengwe; Efs 4:11,12). Kama
mlivyo fundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi aliye mhudumu mwaminifu wa kristo
kwa ajili yenu. Kol 1:7).Taz 1)Tim 1:12). 2)Tim 4:5). Katika sura hizi na misitari hii katika biblia
huonyesha kwamba, uongozi ni huduma ya kuwatumikia watu unao waongoza. Katika
tafsiri ya kiyunani neno kuhudumu humaanisha kutumikia yaani mtu anayewahudumia
wengine yaani ndiye anayewatumikia.
Hata hivyo, iwapo tumekwisha kujifunza
mambo hayo yote ya uongozi lakini tukashindwa kuwaongoza watu wa Mungu kwa
upako mkamilifu ulio katika Yesu kristo, yote yanakuwa ni sifuri. Pasipo Roho
wa Mungu kutia mafuta huduma yetu ya uongozi, hatutaweza kueneza habari njema
ya injili inavyotakiwa. Na bila kuacha kelele na malumbano ya kushindania
uongozi, kutokuwa na roho ya msamaha, uadui, majivuno na nk, Roho mtakatifu
hawezi kwenda pamoja nasi katika uongozi wetu. Badala yake, yatakuwa matokeo ya
nguvu ya mwili pasipo na matunda ya kudumu. Ni mhimu mno kwamba viongozi wa
kanisa kutembea katika utakatifu na kutegemea nguvu ya Roho mtakatifu na nguvu
hii hupatikana tu katika maisha matakatifu. Si kila mtu aniambiae Bwana Bwana atakaye ingia katika ufalme wa
mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba [siyo afanyae uchungaji tu au
askofu]..yangu aliye mbingini.Math 7:21). Theolojia bila Roho
mtakatifu, hatuwezi kuongoza ipasavyo bali Roho mtakatifu ndiyo dira nakiongozi
wetu mkuu. Taz rum 8:14).
Kwa kuwa Mungu hutuhesabu sisi wote kuwajibika, tunahitaji tujuwe
wajibu wetu wa kutambua uongozi sahihi ambao unatufaa sisi kuufaata. Nabii
Yeremia alitoa unabii juu ya wachungaji walioliharibu kanisa la Bwana akisema.
Wachungaji wengi wameliharibu shamba langu la mizabibu, wamelikanyaga fungu
langu chini ya miguu yao, wamefanya fungu zuri kuwa jangwa la ukiwa wamelifanya
kuwa ukiwa, na kwakuwa ni ukiwa linanililia;……Yere 12:10,11). Mungu
alikuwa akizungumza kupitia nabii Yeremia juu ya uongozi wa kidini wa taifa la
Israeli, walikuwa wamewatenda vibaya watu na kuleta uharibifu juu ya nchi.
No comments:
Post a Comment