Sunday, 24 December 2017
New
Karibu Mponeja Blog
About Editorial Staff
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Mafunzo
Labels:
Mafunzo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

Tunaendelea na somo letu kuhusu kiongozi bora wa kiroho;
ReplyDeleteMpendwa katika Bwana, napenda kukukalibisha ili tuendelee na makala yetu inayohusu mafundisho ya biblia kuhusu uongozi bora wa kiroho.
Kiongozi bora wa kiroho ni Yule anayejitoa kwa moyo wa upendo kuwatumikia anaowaongoza bila kulazimishwa. Uongozi wa kiroho siyo kutawala watu. Na kuwaamrisha watu kutii matakwa yako binafsi. Bali uongozi wa kweli wa kiroho ni kuwaelekeza watu kwa moyo wa upendo bila kuangalia hali zao na haliyako kwamba unawazidi nini. Kwa kifupi kiongozi ni mtumwa wa wale anaowaongoza. Akawabia wafalme wa mataifa huwatawala, na wenye mamlaka juu yao huitwa wenye fadhili; lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama Yule atumikaye. Maana aliye mkubwa ni yupi¬¬¬¬? yeye aketiye chakulani, au Yule atumikaye?¬ Siye Yule aketie chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye. Luk 22:25,27]. Yesu alimaanisha kiongozi asiwe mtu mwenye kujisikia kuwa yeye ni kiongozi bali alitaka kiongozi awe ni mtu anayejiona kuwa ni mtumwa maana yake ni mtu aliyetumwa kwa watu wasio wake. Tukijua hilo hatutajiinua na utumishi wetu utakuwa safi mbele za Bwana. Ingawaje biblia inazungumza kuhusu kuonya, kukemea, na kukalipia lakini si katika ukatili wa kibinadamu wenye asili ya ubinafsi na kutosemehe uletao uadui.
Maneno haya karipia, kemea, na onya katika biblia hayamaanishi kufoka , kuwa na jaziba Fulani, kuwa na hasira na mtu furani kwa sababu ya makosa aliyoyafanya nk. Bali humaanisha kuelekeza kwa kina kupitia neno la Mungu. Ukiangalia kwa kina Paulo, anavyotoa maelekezo kwa Timotheo, madhui ya waraka huu huonyesha kabisa Paulo alitaka Timotheo ahubiri na kufundisha neno la kristo kwa uvumilivu wote. Lihubiri neno uwe tayari wakati ukufaao na wakati usio kufaa karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. 2)Tim 4:2,3}.Katika lugha ya asili |kiyunani| maneno haya humaanisha kusihi, kushawishi mtu ahame toka kwenye tabia au mazingira aliyoyazoea, kutoa tahadhari ya mambo yatakayompata mtu mwenye tabia ya asili asipobadilika. Katika tafsiri ya kiyunani cha kisasa, misitari hii humaanisha hivi,hubiri huo ujumbe, sisitiza kutangaza iwe ni wakati wa kufaa au wakati usio faa karipia, onya na himiza….. Kiongozi wa kweli hachaguliwi kwa muonekano wan je tu kuwa anafaa au kwa elimu yake tu ya darasani.
Bali kiongozi wa kiroho huchaguliwa na utatu mtakatifu wa Mungu.Ingawa Mungu anaweza kutumia watu kuchagua kiongozi, lakini lazima Roho mtakatifu aliye kiongozi mkuu apewe nafasi ya kusema na watu na kuwahakikishia kwamba mtu huyu anafaa kuwa kiongozi. Kiongozi wa kiroho hawezi kupatikana paspo Roho mtakatifu. Tunapomluhusu Roho mtakatifu na kumpa nafasi ndani ya roho zetu, yeye huingia na kufanya makao ndani mwetu. Kazi yake kubwa ni kubadili utu wetu wa asili ya dhambi na kutuzaa upya kwa imani nafsi zetu zilizokuwa zimehalibiwa na shetani zinahuishwa na kumtii kristo. Tabia zetu na matendo yetu ya asili yanakufa yaani uchoyo, majivuno,kiburi chuki, unafiki na kila aina ya ubaya yanaondoka kabisa.
Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalumu; ukawaweke juu yao, wawe wakuu…..kut 18:21,22]. Taz mdo 6:3,6].
ReplyDeleteNeno hili kiongozi kwa lugha ya asili yaani kule biblia ilikoanzia /kiyunani humaanisha kiongozi ni mtu anayesahau au kuacha mambo yake au kazi zake kwa ajili ya w engine hii huonyesha ni mtu asiye angalia masirahi katika kazi yake. Tangu mwanzo neno kiongozi, lilitafsiliwa kuwa ni Masihi.Lilitokana na lugha ya kiebrania likimaanisha ‘’mpakwa mafuta’’ neno hili lilitumika kwa wale tu waliokuwa wamechaguliwa na Mungu kwa ajili ya kuwaongoza watu wa Mungu. Waisraeli wa agano la kale, walifanya sherehe ya kupaka mafuta kwa wafalme, makuhani, na mara nyingine kwa manabii mafuta rasimi yalimiminwa kichwani pa mtu ikiwa ishara ya kuwa tangu sasa amekuwa na haki ya kuwa kiongozi, ili kutekeleza huduma iliyolingana na wito wake. Taz kut, 28:41]. 1]fal 1:39. Na 19:16].
Katika nchi za agano jipya zilizokuwa na lugha ya kiyunani, neno la kiebrania ‘’masihi’’ lilitafsiriwa katika kiyunani likawa ‘’kristo” likimaanisha mpakwa mafuta. Hii haimaanishi kwamba kiongozi achukue nafasi ya kristo na kulitumia jina hili kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya kufanya lolote kwa wale anaowaongoza la bali humaanisha kiongozi wa kiroho anatakiwa kuwa wakili bora anayemuwakilisha kristo katika uogozi bora . Tabia na mwenendo wake uwe kama wa kristo. Asitake madaraka kwa manufaa yake na familia yake.
Migogoro mikubwa makanisani, siku hizi inaletwa na viongozi. Viongozi wanaojiita maasikofu na wachungaji, asilimia kubwa ya watu hawa wamekuwa chachu ya maendeleo ya kanisa wamechachua mpaka waumini kwa kuwaingizia roho za uadui. Mchungaji na mchungaji hawapatani wanawalazimisha na wanaowaongoza wawe na chuki juu ya mchungaji Fulani wakitumia sentesi dhaifu kabisa mimi naita sentesi mfu eti wanasema mimi ni baba yenu na ninyi ni wanangu baba akisema lolote mtoto lazima utii na kukubali. Viogozi hawa wanatia huruma kwani kanisa wanakolipeleka si huko kristo anakotaka. Badala ya kutengeneza na kuzalisha viongoz I bora wa kesho wao wanatengeneza nakuzalisha kesi nyingi sana mahakamni zisizokuwa na maana yoyote. Wana hujumu mali za kanisa bila hata hofu ya Mungu wanataka wapewe heshima za kichungaji na za kiasikofu wanatanguliza vyeo vyao mbele kuliko kumtanguliza kristo kwa nje ni watumishi wa Mungu lakini ndani ni mafasayo wakubwa. Tena matendo yao yote huyatenda ili watazamwe na watu. Ni watu wanaopenda kutumia vyeo vyao. Hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu Rabi…….Math 23:6,12)
Ukiangalia sura nzima ya 23 katika mathayo, mwandishi ananukuru kwa kina mafundisho ya Yesu yanayokemea tabia ya watu wanaotaka kutumia madaraka ya uongozi kwa kuwafanya wengine kama mateka. Hawako tofauti na wandishi na mafarisayo wanafiki Ole wenu wandishi na mafarisayo, wanafiki kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni;[kwa kuwawekea masharti magumu]..ninyi wenyewe hamuingii, wala wanaoingia [washrika waliodhamilia]..hamuwaachi waingie. Utakuta mchungaji ameweka mashariti kibao kanisani kwake utadhani anongoza familia yake washirika wanamhofu na kumtetemekea kuliko hata Mungu wanaona ni afadhali kumkosea Mungu kuliko mchungaji. Mchungaji mwema huwafanya watu kuwa rafiki ili wamueleze matatizo na udhaifu wao unaowafanya kushindwa kuwa wakamilifu mbele za Bwana ili auchukue mbele za Bwana kwa maombi siyo kufoka tu na kuwatishia laana. Mchungaji mmoja alitumia dakika30 madhabahuni akimfokea mshirika mmoja alipitia mlango wa pembeni anaotumia mchungaji kuingia kanisani baada ya ibaada mtu huyo hakuludi tena kanisani na mchungaji hakuonekana wala kuumiza kichwa chake kwa ajili ya mshirika huyo kilchofaata ni mchungaji huyo kusema huyo ni mpagani kabisa. Ni vizuri kuwa na utaratibu, katika ibaada zetu lakini masherti yasitufanye kuwakosesha wengine wasmwabudu Mungu kwa furaha na amani kwa kigezo kuwa eti wewe ndiyo mchungaji eti hata kama nibaki peke yangu kazi itaenda tu hapana. Tangu mwanzo Mungu wetu ni wa watu wengi kwa nini asingekomea na Adamu peke yake aliyemuumba lakini akataka kupitia Adamu watu wakaongezeke na kuijaza nchi.
ReplyDeleteWala msiitwe viongozi; kiongozi wenu ni mmoja naye ndiyo Kristo Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu, 23:10,12). Siyo kwamba atakuwa baba yenu kama watu walivyolibadilisha neno hili na kujiita mababa wa kanisa. Makusudi ya sura hii nzima yanapatikana kwenye mstari wa 12. Ingawa Yesu alisema maneno mengi kuwaonya viongozi waliokuwa wakiwabebesha wengine mizigo mizito na wao hawawezi kuibeba, wanajihesabia haki siku zote, msingi na kusudi kuu la mafundisho yake lilikuwa ni hili hapa. Na yeyote atakayejikweza, atadhiliwa; na yeyote atakayejidhili, atakwezwa 23:12).
Maneno haya yesu anazungumza juu ya viongozi sio washirika. Ingawa alikuwa anazungumza na viongozi wa sheria, asilimia kubwa ya wachungaji wa leo, ndiyo wanayafanya hayo wamekuwa wakandamizaji wakubwa wa washrika na wachungaji wenye huduma ndogo bila hata msaada wowote wakijisema wanasimamia maadili ya wokovu. Lakini bado wanatapeli mali za washirika na kujitangaza wamebarikiwa na Mungu. Kama ni Mungu kwa nini aswabariki na hao wanao leta sadaka?. Angalia kisa cha mchungaji mmoja wa kanisa furani la kipentekoste
Alimuita mzee wa kanisa ofisini kwake akitaka kumtuma dukani kwakuwa mchungaji huyu alitaka kitu hicho kiwahi, mzee wa kanisa kwa kuwa alikuwa wa makamo, aliangalia kijana mwepesi ili akimbie haraka na kuludi. Baada ya mda kidogo mchungaji alitoka nje akmuita na kumuuliza Yule mzee na yeye mzee hakuwa na wasiwasi akajibu akajibu akasema nimemwagiza kijana ili awahi. Mchungaji alimnasa kofi la shavu kwakuwa mzee huyu hakuwa na maadalizi ya kichpo hicho alishika shavu lake kwa maumivu makali mbele ya watu, akazunguka nyuma ya jengo la kanisa. Hii yote ni kujiona kuwa mimi ni kiongozi. Sifa wanayotakiwa kuwa nayo wafuasi wa kristo ni utumishi siyo kutumikiwa
Kiongozi wa kanisa, mwenye kazi ya uchungaji, ambao ni tofauti na mashemasi huitwa mhudumu pia. Naye alitoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisiti; na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha [siyo kuwasambaza]..watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa kristo ujengwe; Efs 4:11,12). Kama mlivyo fundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi aliye mhudumu mwaminifu wa kristo kwa ajili yenu. Kol 1:7).Taz 1)Tim 1:12). 2)Tim 4:5). Katika sura hizi na misitari hii katika biblia huonyesha kwamba, uongozi ni huduma ya kuwatumikia watu unao waongoza. Katika tafsiri ya kiyunani neno kuhudumu humaanisha kutumikia yaani mtu anayewahudumia wengine yaani ndiye anayewatumikia.
ReplyDeleteHata hivyo, iwapo tumekwisha kujifunza mambo hayo yote ya uongozi lakini tukashindwa kuwaongoza watu wa Mungu kwa upako mkamilifu ulio katika Yesu kristo, yote yanakuwa ni sifuri. Pasipo Roho wa Mungu kutia mafuta huduma yetu ya uongozi, hatutaweza kueneza habari njema ya injili inavyotakiwa. Na bila kuacha kelele na malumbano ya kushindania uongozi, kutokuwa na roho ya msamaha, uadui, majivuno na nk, Roho mtakatifu hawezi kwenda pamoja nasi katika uongozi wetu. Badala yake, yatakuwa matokeo ya nguvu ya mwili pasipo na matunda ya kudumu. Ni mhimu mno kwamba viongozi wa kanisa kutembea katika utakatifu na kutegemea nguvu ya Roho mtakatifu na nguvu hii hupatikana tu katika maisha matakatifu. Si kila mtu aniambiae Bwana Bwana atakaye ingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba [siyo afanyae uchungaji tu au askofu]..yangu aliye mbingini.Math 7:21). Theolojia bila Roho mtakatifu, hatuwezi kuongoza ipasavyo bali Roho mtakatifu ndiyo dira nakiongozi wetu mkuu. Taz rum 8:14).
Kwa kuwa Mungu hutuhesabu sisi wote kuwajibika, tunahitaji tujuwe wajibu wetu wa kutambua uongozi sahihi ambao unatufaa sisi kuufaata. Nabii Yeremia alitoa unabii juu ya wachungaji walioliharibu kanisa la Bwana akisema. Wachungaji wengi wameliharibu shamba langu la mizabibu, wamelikanyaga fungu langu chini ya miguu yao, wamefanya fungu zuri kuwa jangwa la ukiwa wamelifanya kuwa ukiwa, na kwakuwa ni ukiwa linanililia;……Yere 12:10,11). Mungu alikuwa akizungumza kupitia nabii Yeremia juu ya uongozi wa kidini wa taifa la Israeli, walikuwa wamewatenda vibaya watu na kuleta uharibifu juu ya nchi.