- MPONEJA BLOG

Latest

Monday, 12 February 2018

            MAKUSUDI YA YESU KRISTO KUJA ULIMWENGUNI;
Tangu mwanzo, biblia hufundisha na kueleza kwa kina kuwa Yesu ni mwana wa Mungu. Zaidi ya miaka 2000 iliyopita, alitokea kwenye sura ya hisitoria. Hata kama alitungwa kwa njia pekee ya kimungu, alizaliwa katika ulimwengu na alikuwa na kufikia utu uzima kama watu wengine, lakini alikuwa tofauti na mtu mwingine yoyote. Hakuwa mtu wa kawaida. Kwa hiyo, kabla ya kujua makusudi ya ujio wake ni vyema kumuelewa asili yake.
Biblia inasema bikira alichukua mimba kwa uwezo wa Roho mtakatifu na akamzaa. Alikuwa ni Mungu mwenyewe, aliyekuja duniani kwa namna ya kibinadamu. Alikuwa mwana wa aliye juu  taz Luk 1:26,35).
          Hapo mwanzo kulikuwapo neno[Yesu] naye neno alikuweko kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu, naye alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa wema na kweli’’Yoh 1:1,14).
    Biblia inaweka wazi kusudi maalum la Yesu kuja ulimwenguni kuwa ni kwa ajiri ya  wanadamu wote endapo wataamini kazi yake ya ukombozi
Hebu tuangalie makusudi sita ambayo hutokana na neno moja tu ukombozi kwa saqbabu kristo amekuja kwa kazi moja tu ya ukombozi.
                               A   ALIKUJA KWA KUSUDI MAALUMU;
1.     Kumkoboa mwanadamu kutkana na nguvu za shetani.
kwa kuwa mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. Luk 19:10). Taz Kol1:13).
2.     Kutoa uhai wake kama kama fidia.
Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa bali kutumika na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi. Mt 20:28).
3.      Kuzivunja kazi za shetani katika maisha yetu.
Atendaye dhambi ni wa Iblisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. 1)Yoh3:8).
4.      Kutupa uzima wa milele . Na huu ndiyo ushuhuda ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika mwanawe Yesu aliyenaye mwana anao huo uzima; asiye naye mwana wa Mungu hana huo uzima.1)Yoh 5:11,12 taz Yoh 3:16). 10:10).
5.      Kutupa uwezo wa kuzaliwa upya;
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. Yoh 1:12).
  
6.      Kurejesha ushirika wetu na Mungu Baba;
Hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi; na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na mwana wake Yesu kristo. 1)Yoh 1:3).
          B. ALKUJA KUTUONYESHA JINSI MUNGU ALIVYO;
                                                                                                                                              
                 Kusudi jingine la kristo kuja ulimwenguni ni yeye kutuonyesha Mungu alivyo, upendo wake, na tabia yake kusudi hili la pili litatufanya kuelewa kuwa Mungu wetu  ni wa upendo, huponya, na hutoa Baraka kupitia kristo Yesu.
Kama mngalinijua mimi [Yesu] mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemuona…Aliyeniona mimi amemuona Baba; basi wewe wasemaje utuonyeshe Baba? Baba yu ndani yangu? . Haya maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba ndani yu ndani yangu. Yoh14:7,11).
1.     Alituonyesha upendo wa Mungu;
      Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye. Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu bali kwamba yeye alitupenda sisi , akamtuma mwanaye kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu 1)Yoh 4:9,10). Taz Rum 5:8).
  
2.     Alituonyesha nguvu za Mungu;
Kupitia jina lake alituonyesha nguvu ya Mungu hushuka na kuleta uponyaji aliponya wagonjwa , viwete na vipofu. Na habari zake zikaenea katika sham yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalmbali na mateso, wenye pepo na wenye kifafa na wenye kupooza; akawaponya. Mth 4:24). Taz Yoh 9:1,7).
  Kupitia yeye miujiza mingi mno ilitendeka. Hii ilimaanisha kwamba kila anayemwamini kikwelikweli  kupitia jina kake atafanya haya yote. Pasingelikuwa kristo watu tusingalijua nguvu hii ya ukombozi ulimwengu huu ungaltawaliwa na mapepo ya kila aina.  Alifufua wafu, alituliza bahari, altoa pepo, alifanya muujiza wa chakula, kila aina ya tatizo lililogusa moyo wa mwanadamu, ukaumia alilishughulikia ili tu mwanadamu amwamini kwamba yeye amekuja kwa ukombozi. Maandiko ni mengi mno katika biblia yanayozungumza habari ya miujiza ya Yesu kristo kuhusu ukombozi wa wanadamu.
           C.  KUSHIRIKI MATESO PAMOJA NASI;
                                                                  
Wakati wa maisha ya Yesu haapa duniani, Yesu alijua kabisa matatizo na shida za maisha ya hapa dunani. Alijua change moto zote zinazo tukabili, na vile tunvyojisikia, tunapokuwa katika hali ya dhiki. Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijalibiwa  sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.Ebr 4:15). Taz Mth 8:17).
                                                                                                                                
Kwa sababu dunia nzima [wanadamu] ilisitahili hukumu ya kifo, kwa sababu ya uasi wa tangu Adamu, Yesu kristo alikuja ili afe msalabani kwa ajili  yetu kwa sababu ilikuwa kwa njia ya kifo cha msalaba, Mungu aukomboe ulimwengu kwa kila anayeamini tu. Kwa hiyo, Yesu alikufa kwa ajili yetu na kwa niaba yetu soma mark 15:16,39). Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti; ili tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi,tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa 1)pet 2:24). Taz Isa 53:5,6). Kifo cha Yesu kinabadilisha kabisa hukumu liiyokuwa ikitukabili. Mabadiliko haya, ni kwa Yule tu anayemwamini Yesu kristo na kumpokea na kutembea katika nyendo zake.
           
Baada ya kukaa siku tatu kaburini, Mungu alimfufua mwanaye kutoka kwenye mauti  Lakini Mungu kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu war oho katika kristo Yesu Efs2:4,6).Taz Rum 6:4). Kupitia hatua hizi zote, Yesu kristo alipomaliza kazi yake hapa duniani, aliludi mbinguni kwa Baba yake.Hii yote alifungua mlango wa mbinguni kwa ajili yetu. Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai ipitayo katika pazia yaani, mwili wake na tukaribie wenye moyo wa kweli kwa utimilifu wa imani. Ebr 10:19,22). Taz Yoh 14:1,3).
                
No comments:

Post a Comment