MAKUSUDI YA YESU KRISTO KUJA
ULIMWENGUNI;
Tangu
mwanzo, biblia hufundisha na kueleza kwa kina kuwa Yesu ni mwana wa Mungu.
Zaidi ya miaka 2000 iliyopita, alitokea kwenye sura ya hisitoria. Hata kama
alitungwa kwa njia pekee ya kimungu, alizaliwa katika ulimwengu na alikuwa na
kufikia utu uzima kama watu wengine, lakini alikuwa tofauti na mtu mwingine
yoyote. Hakuwa mtu wa kawaida. Kwa hiyo, kabla ya kujua makusudi ya ujio wake
ni vyema kumuelewa asili yake.
Biblia inasema bikira alichukua mimba
kwa uwezo wa Roho mtakatifu na akamzaa. Alikuwa ni Mungu mwenyewe, aliyekuja
duniani kwa namna ya kibinadamu. Alikuwa mwana wa aliye juu taz Luk 1:26,35).
Hapo
mwanzo kulikuwapo neno[Yesu] naye neno alikuweko kwa Mungu, naye Neno alikuwa
Mungu, naye alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu
kama wa mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa wema na kweli’’Yoh 1:1,14).
Biblia inaweka wazi kusudi maalum la Yesu
kuja ulimwenguni kuwa ni kwa ajiri ya wanadamu wote endapo wataamini kazi yake ya
ukombozi
Hebu
tuangalie makusudi sita ambayo hutokana na neno moja tu ukombozi kwa saqbabu
kristo amekuja kwa kazi moja tu ya ukombozi.
1. Kumkoboa mwanadamu kutkana na nguvu za shetani.
kwa kuwa mwana wa Adamu
alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. Luk 19:10). Taz Kol1:13).
2. Kutoa uhai wake kama kama fidia.
Mwana wa Adamu
asivyokuja kutumikiwa bali kutumika na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi. Mt
20:28).
3. Kuzivunja kazi za shetani katika maisha yetu.
Atendaye dhambi ni wa
Iblisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo kwa kusudi hili mwana wa
Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. 1)Yoh3:8).
4. Kutupa uzima wa milele . Na huu ndiyo ushuhuda ya kwamba Mungu
alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika mwanawe Yesu aliyenaye mwana
anao huo uzima; asiye naye mwana wa Mungu hana huo uzima.1)Yoh 5:11,12 taz Yoh
3:16). 10:10).
5. Kutupa uwezo wa kuzaliwa upya;
Bali wote waliompokea
aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
waliozaliwa si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya
mtu, bali kwa Mungu. Yoh 1:12).
6.
Kurejesha
ushirika wetu na Mungu Baba;
Hilo tuliloliona na
kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi; na
ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na mwana wake Yesu kristo. 1)Yoh
1:3).
B. ALKUJA KUTUONYESHA JINSI MUNGU
ALIVYO;
Kusudi jingine la kristo kuja
ulimwenguni ni yeye kutuonyesha Mungu alivyo, upendo wake, na tabia yake kusudi
hili la pili litatufanya kuelewa kuwa Mungu wetu ni wa upendo, huponya, na hutoa Baraka
kupitia kristo Yesu.
Kama mngalinijua mimi [Yesu] mngalimjua na Baba; tangu sasa
mnamjua, tena mmemuona…Aliyeniona mimi amemuona Baba; basi wewe wasemaje
utuonyeshe Baba? Baba yu ndani yangu? . Haya maneno niwaambiayo mimi siyasemi
kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki
ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba ndani yu ndani yangu. Yoh14:7,11).
1.
Alituonyesha
upendo wa Mungu;
Katika hili pendo la Mungu
lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate
uzima kwa yeye. Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu bali kwamba
yeye alitupenda sisi , akamtuma mwanaye kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu 1)Yoh
4:9,10). Taz Rum 5:8).
2.
Alituonyesha
nguvu za Mungu;
Kupitia jina lake alituonyesha nguvu ya Mungu hushuka na kuleta uponyaji
aliponya wagonjwa , viwete na vipofu. Na habari zake zikaenea katika sham yote;
wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalmbali na mateso,
wenye pepo na wenye kifafa na wenye kupooza; akawaponya. Mth 4:24). Taz Yoh
9:1,7).
Kupitia yeye miujiza mingi mno ilitendeka.
Hii ilimaanisha kwamba kila anayemwamini kikwelikweli kupitia jina kake atafanya haya yote.
Pasingelikuwa kristo watu tusingalijua nguvu hii ya ukombozi ulimwengu huu
ungaltawaliwa na mapepo ya kila aina.
Alifufua wafu, alituliza bahari, altoa pepo, alifanya muujiza wa
chakula, kila aina ya tatizo lililogusa moyo wa mwanadamu, ukaumia alilishughulikia
ili tu mwanadamu amwamini kwamba yeye amekuja kwa ukombozi. Maandiko ni mengi
mno katika biblia yanayozungumza habari ya miujiza ya Yesu kristo kuhusu
ukombozi wa wanadamu.
C. KUSHIRIKI MATESO PAMOJA NASI;
Wakati wa
maisha ya Yesu haapa duniani, Yesu alijua kabisa matatizo na shida za maisha ya
hapa dunani. Alijua change moto zote zinazo tukabili, na vile tunvyojisikia,
tunapokuwa katika hali ya dhiki. Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza
kuchuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijalibiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila
kufanya dhambi.Ebr 4:15). Taz Mth 8:17).
Kwa sababu dunia nzima [wanadamu]
ilisitahili hukumu ya kifo, kwa sababu ya uasi wa tangu Adamu, Yesu kristo
alikuja ili afe msalabani kwa ajili yetu
kwa sababu ilikuwa kwa njia ya kifo cha msalaba, Mungu aukomboe ulimwengu kwa
kila anayeamini tu. Kwa hiyo, Yesu alikufa kwa ajili yetu na kwa niaba yetu
soma mark 15:16,39). Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika
mwili wake juu ya mti; ili tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi,tuwe hai kwa mambo
ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa 1)pet 2:24). Taz Isa 53:5,6). Kifo
cha Yesu kinabadilisha kabisa hukumu liiyokuwa ikitukabili. Mabadiliko haya, ni
kwa Yule tu anayemwamini Yesu kristo na kumpokea na kutembea katika nyendo
zake.
Baada ya kukaa siku tatu kaburini, Mungu alimfufua mwanaye
kutoka kwenye mauti Lakini Mungu kwa kuwa ni mwingi
wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda. Akatufufua pamoja naye,
akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu war oho katika kristo Yesu
Efs2:4,6).Taz Rum 6:4). Kupitia hatua hizi zote, Yesu kristo
alipomaliza kazi yake hapa duniani, aliludi mbinguni kwa Baba yake.Hii yote
alifungua mlango wa mbinguni kwa ajili yetu. Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu
kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai ipitayo katika
pazia yaani, mwili wake na tukaribie wenye moyo wa kweli kwa utimilifu wa
imani. Ebr 10:19,22). Taz Yoh 14:1,3).

No comments:
Post a Comment